Wabunge wa Yanga wafaya uchaguzi wa Uongozi Mpya


Wabunge wa Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania ambao ni wanachama wa Timu ya Yanga, wamekutana leo mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu timu yao ikiwa ni pamoja na kuupata uongozi wa Tawi lao kwa muda huu wa mpito. Wabunge hao wanaYanga, wamefanikisha zoezi la kuchagua viongozi wa mpito wa Tawi lao.


Katika kikao hicho, Waliwachagua Mh. Venance Mwamoto kuwa Mwenyekiti wa Tawi hilo, huku nafasi ya umakamu ikishikwa na Mh. Ridhiwani Kikwete, Mh. Hafidh Ally Tahir -Katibu Mkuu, Mh. Hamidu Bobali -Naibu Katibu, Mh. Martha Mlata-Mweka Hazina na Mh. Abdallah Ulega anakuwa Mweka Hazina Msaidizi.



Kwa upande wa kamati tendaji, Wajumbe wake ni kama ifuatavyo. Mh. Grace Kihwelu, Mh. Halima Mdee, Mh. Seifu Gulamali, Mh. Gibson Meiseyeki, Mh. Issa Mangungu pamoja na Mh. Dotto Biteko



Katika Baraza la Wazee wa Yanga Bungeni, kuna Mh. Freeman Mbowe, Mh. Mwigulu Nchemba, Mh. Hawa Ghasia pamoja na mjumbe mmoja ambaye atatoka Zanzibar.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo