Wafanyabiashara wafunga Barabara kwa Mawe Mkoani Morogoro

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limelazimika kutoa mawe na magogo yaliyowekwa kufunga barabara za mitaa na wafanyabiasha waliosadikiwa kuwa ni wauza nguo maarufu kwa (Mitumba) baada ya halmashauri ya Morogoro kuanza uvunjaji wa soko kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa.

Hali hiyo imemfanya mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi.Regina Chonjo pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kutoka ofisini na kuzunguka kwa gari kujionea halihalisi kisha kufanya mazungumzo na viongozi wa wafanyabiasha ofisini kwake ambapo amelaani vikali tabia hiyo huku akimuagiza mkurugenzi wa halmashauri kushughulikia changamoto walizoeleza wafanyabiashara hao.

Wakizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya  wafanyabiashara wameuomba uongozi huo kupewa maeneo mengine kwakuwa eneo walilopangiwa ni dogo na haliwezi kutosheleza kukaa wafanya biashara wote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo