Shekhe
Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir
(Mwenye kofia Nyeupe katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
SHEKHE
Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir
pamoja amelaani vikali tukio la kinyama lililotokea Mei 17 mwaka huu
katika Msikiti wa Ibanda Mkolani, Masjid Rahmaan mkoani Mwanza.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na hakivumiliki.
Tukio
hilo lilitokea May 17 mwaka huu na kusababisha mauaji ya waumini watatu
wa Msikiti wa Ibanda Mkolani waliokuwa katika Ibada miongoni mwao akiwa
ni Imam wa Msikiti huo ikiwa na wengine kujeruhiwa.
"Kwaniaba
ya Baraza kuu la Waislam wa Tanzania(Bakwata) tunalaani vikali tukio
hili pamoja na kuwataka Waislam wawe watulivu katika kipindi hiki
kigumu" Amesema Shekhe Zuberi.
Amewaomba
Waislam na wananchi kwa ujumla kuvipa ushirikiano wa hali na mali
vyombo vya usalam ili hatimae kuwapata waharifu hao ili waweze
kufikishwa katika vyombo vya Sheria.
Shekhe
Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir
akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, na kulaani
kitendo cha mauaji ya watu wasio na hatia katika Msikiti huko Mkoani
Mwanza. Kulia ni Msaidizi katika ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe,
Ally Khamisi Ngeruko. na Kushoto ni Shekhe, Abuubakari Kharid.
Baadhi
ya waamini wa dini ya Kiislamu pamoja na waandishi wa habari
wakimsikiliza Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania,
Aboubakar Zubeir jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.