Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mh. Godbles Lema ameshauri
kufungwa kwa vifaa maalum vinavyopima ulevi ndani ya bunge ilikulinda
heshima ya Muhimili huo wa bunge.
Katika mahojiano Maalum na ITV Dar es Salaam waziri huyo kivuli
pamoja na mambo mengine amepongeza uamuzi wa rais wa kumfuta kazi
aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nje Charles Kitwanga huku akisema
ni dhahiri kiongozi huyo amechafua hadhi ya wizara ya mambo ya ndani ya
nchi.
Katika Mahojiano hayo Lema amekiri kitendo cha unywaji wa Pombe
kupitiliza kwa kiongozi ni utovu wa nidhamu jambo ambalo huenda likazidi
kushusha hadhi ya bunge ambalo ni Mahususi kwa kutunga sheria na
kuisimamia Serikali.
Haya yanakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya taarifa ya Ikulu ya
Dar es Salaam kutangaza kumtimua kazi aliyekuwa waziri wa mambo ay nadni
ya nchi baada ya kuingia bungeni na kujibu swali la wizara yake
kimakosa huku akiwa amelewa.