BREAKING NEWS: MTAFARUKU BUNGENI WAMLAZIMU SPIKA MAKINDA KUAHIRISHA BUNGE USIKU HUU

Kumetokea mtafaruku bungeni Dodoma usiku huu baada ya kutokea mvutano miongoni wa wabunge kuhusu viongozi wanaopaswa kuwajibika kutokana na sakata la Escrow.
Baadhi ya wabunge hususani kutoka vyama vya upinzani wametaka wahusika wawajibishwe ikiwemo kuachia ngazi, huku wale wabunge wanaodaiwa kuwa wa CCM wakionesha kutounga mkono maamuzi hayo na pia wabunge hao wakidai wanawalinda baadhi ya viongozi.
Spika wa bunge Anne Makinda ameahirisha kikao cha Bunge hivi punde saa tano kasoro usiku huu, baada ya kutokea kwa  sintofahamu hiyo ya wapinzani kudai Waziri Muhongo analindwa.

Baadhi ya wabunge wamepiga kelele na kuimba bungeni, Spika ameahirisha bunge hadi watakaposhauriana


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo