TCCIA YATILIANA SAINI NA JESHI LA POLISI


Chemba ya biashara, viwanda na kilimo nchini,TCCIA imetiliana saini ya makubalianao na jeshi la polisi nchini ya kuendeleza ubia kati ya jeshi hilo na sekta binafsi katika ulinzi na usalama kwa wadau wa chemba hiyo.

Wakitiliana saini hati ya makubalianao hayo jijini DSM ,Rais wa chemba hiyo Mhandisi PETER CHISAWILLO na kamishna wa operesheni maalum PAUL CHAGONJA wamesema hatua hiyo imefikiwa ni katika kuendeleza na kutekeleza maazimio ya mkutano uliopita wa SMART PARTNERSHIP na kuongeza kuwa amani na utulivu vikipotea hakuna maendeleo ya kiuchumi,ambapo pia makubaliano hayo ni katika kuadhimisha miaka 25,TCCIA.

Aidha chemba hiyo katika wiki hii ya kusheherekea kutimiza miaka 25 ya kuzaliwa ambayo kilele chake oktoba 28 mwaka huu itafanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ya utoaji wa tuzo kwa waanzilishi wa TCCIA,watu binafsi na taasisi nyingine zilizosaidia chemba hiyo kufikia ilipo sasa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo