POLISI WAPONGEZWA KWA KUWAUA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI MKOANI GEITA


Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya Sanlg yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la Mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert Kulwa(59) mkazi wa Tambukaleli mjini Geita.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa Mpesa na kufariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Amesema mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo  wa  Mpesa.

Kamanda ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi  cha shilingi millioni moja na laki nane  na   kumpora  bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo.

Aidha majambazi hao walikuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.

Jeshi la polisi lilipata taarifa muda mfupi  ambazo  zilizotolewa na raia wema ambapo kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao walifanikiwa kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.

Wakiwa wanakimbizana, majambazi hao walipowaona askari, jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza  kuwashambulia askari kwa risasi lakini dereva wa polisi alimfuata moja kwa moja na kumgonga kwa gari jambazi huyo na kufariki papo hapo.
Baada ya hapo jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza kumfukuza wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshambulia na alifariki wakati anakimbizwa hospitali.

Taharuki hiyo iliukumba mji wa Geita kwa masaa takribani 3 kabala hawajakamatwa majira ya saa 2 .

Baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya tukio hilo huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo