Mtoto azaliwa akiwa na vichwa viwili

Mwanamke mmoja mjamzito mkazi wa kijiji cha Chakonka Wilaya ya Uvinza, Kigoma amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili na baada ya muda mfupi mtoto huyo alifariki.
Ilidaiwa kuwa awali alikwenda kwenye kituo cha afya lakini hakupatiwa matibabu inavyotakiwa na hatimaye alikimbizwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa ambapo alijifungua wa upasuaji.
Mume wake alisema mkewe alipata uchungu saa 8 usiku na kukimbizwa na usafiri wa boti usiku huo hadi kituo cha ifya ingawa hawakuweza kumsaidia na Baadaye alipelekwa hospitali ya rufaa Maweni.
Akithibitisha tukio hilo Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Shija Ganai alisema walimpokea mganga huyo saa 11 jioni na walipomchunguza walibaini mtoto ametanguliza miguu ndipo wakaamua kumfanyia upasuaji.
Anasema walibaini kuwa mtoto ana vichwa viwili ndiyo sababu ilichangia kufariki dunia mapema kutokana na kubanwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo