Baada ya Mgombea ubunge Jimbo la Ludewa kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Bwana Bathromeo Msambichaka Mkinga hapo septemba 3 mwaka huu kuzindua kampeni zake mjini Ludewa,hapo Jana Ameanza kujichimbia vijijini kusaka kura kwa wananchi.
Mkutano wa Kwanza Mara baada ya uzunduzi huo ameufanya katika kijiji cha Lugarawa ambako pamoja na mambo mengine mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia Chadema bwana George Mlelwa ametumia nafasi hiyo kuweka wazi mipango yake ndani ya kata hiyo endapo Atachaguliwa.
Akizungumza katika kijiji hicho mgombea huyo wa Udiwani bwana Mlelwa amesema pamoja na ahadi hewa ambazo Wagombea mbalimbali waliopita wameshindwa kutekeleza basi kupitia chadema kwa kushirikiana na Mbunge wao atahakikisha anakwenda kupambana na changamoto hizo.
Bwana Mlelwa amesema endapo wakazi wa kata hiyo watamchagua kuongoza kata hiyo basi atakwenda kukabiliana na matatizo ya uhaba wa maji, Afya, Elimu pamoja na kuhakikisha umeme unafika kila kijiji tofauti na sasa.
Emmanuel kayombo ni kaimu katibu wa chadema Mkoa wa Njombe ambaye amesema suala la Ccm kutumia Ilani ya chadema katika mambo muhimu kama elimu bure, Afya pamoja na masuala ya kufanya mabadiliko ya katiba ya Tanzania na kuwadanganya wananchi kuwa ndio wamedhamiria kuwakomboa wananchi ni kuwalaghai.
Meneja wa kampeni hizo bwana Edward kazimoto amesema Mara baada ya chadema kufanikiwa kuingia madarakani Watakwenda kuvunja mikataba feki ya madini na kusaini upya kwa maslahi ya
watanzania.
Kwa upande wake mgombea ubunge huyo bwana Msambichaka Mkinga amesema kuwa amelazimika kuingia kwenye Kinyang'anyiro hicho kutokana na haki zao kwenda mashakani kwa mikataba feki inayowezakusainiwa endapo wataendelea kuchagua chama tawala.
Suala la kufungua taasisi za fedha ni miongoni mwa mambo ambayo amesema atakwenda kushughulika nayo kwani anaamini uchumi wa kweli unatokana na mikopo ambayo imekuwa inariba ndogo kwa wananchi.

Na Gabriel Kilamlya, LUDEWA
