Kwa Siku ya Tatu Sasa Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bwana Bathromeo Msambichaka Mkinga Ameendelea Kujichimbia Katika Vijiji na Kata Mbalimbali Kutafuta Kura Kwa Wananchi Mara Baada ya Kuzindua Rasmi Kampeni Zake Hapo Septemba 3 Mwaka Huu.
Septemba Tano Mwaka Huu Mgombea Ubunge Huyo Amewasili na Kufanya Mkutano na Wakazi wa Kijiji na Kata ya Mavanga Ambako Kumeonekana Kuendelea Kukumbwa na Changamoto Lukuki Ambazo Zinakosa Mtu wa Kuzitatua.
Awali Wakizingumza Katika Mkutano Huo Uliofanyika Katika Kitongoji Cha Mbugani Katika Eneo la Muungano Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA Ngazi ya Mkoa Pamoja na Mgombea Udiwani Kata ya Mavanga Bwana Elneus Kalomo Mgimba Wamesema Kuwa Matatizo Mengi ya Wakazi wa Kata Hiyo Yanashindwa Kutekelezwa Kutokana na Mfumo wa Chama Tawala Ambao Unatajwa Kujilimbikizia Mali Kupitia Viongozi Wake Badala ya Wananchi.
Aidha Mgombea Udiwani Huyo Bwana Elneus Kalomo Mgimba Amesema Anachotaka Si Kwenda Kuwanunulia Pombe Wazee Katika Kijiji Hicho na Mwishowe Zinakwisha Bali Anataka Kwenda Kuwafundisha Kutafuta Fedha Zitakazo Wasaidia Hata Kama Hayupo.
Amesema Matatizo ya Maji,Afya na Elimu Ambayo Yamekuwa Kikwazo Katika Shughuli za Maendeleo Atakwenda Kukabiliana Nayo Endapo Wananchi Watamchagua Katika Uchaguzi Mkuu Hapo Oktoba 25 Mwaka Huu.
Amesema Hatua ya Viongozi wa Juu Katika Chama Cha Mapinduzi CCM Kama Edward Lowasa na Fredrick Sumaye Kuamua Kuhama Chama Hicho Kunatokana na Manyanyaso Yaliyopo Ndani ya CCM Jambo Ambalo Hata Wananchi Wamekuwa Wakiyapata Kwa Miaka Yote Tangu Uhuru wa Tanzania.
Mzee Bonface Nyigu Maarufu Kama Mzee Mgongo Mwenye Umri wa Miaka 94 Ambaye Hivi Sasa Amehamia CHADEMA Baada ya Kukimbia CCM Kwa Kile Alichokieleza CCM Imeshindwa Kuwasaidia Wazee Amesema Kwa Miaka Mingi Sasa Wazee Wamekuwa Wakipata Adha Kubwa Katika Masuala Mbalimbali Yakiwemo ya Afya Licha ya Serikali Kuahidi Bila Utekelezaji.
Mzee Nyigu Amesema Kuwa Serikali ya Chama Tawala Imekuwa Ikitoa Ahadi za Wazee Kupata Huduma ya Afya Bure Lakini Utekelezaji Wake Umekuwa Duni Hainabudi Kuitupilia Mbali Ifikapo Oktoba 25 Mwaka Huu Katika Uchaguzi Mkuu.


