Wananchi na wafanyabiashara wa kijiji cha Makusi kata ya Itundu wilayani
Makete mkoani Njombe wameulalamikia uongozi wa kata hiyo kuahidi kujenga soko lakini ahadi
hiyo haijatimia
Wakizungumza na mwandishi wa eddy blog baadhi ya wananchi waliojitambulisha kwa majina ya
Christina Mbwilo na Sayuni Mbilinyi wamesema kuwa kijiji hicho hakina soko la
kudumu kwa muda mrefu ambapo watu hufanya biashara sehemu yeyote
Wamesema kwa sasa soko linalotumika kwa muda halina vyoo hali inayopelekea
watumiaji wa soko hilo kujisaidia kwenye vyoo vya nyumba za majirani wa soko
hilo hali inayosababisha kero kwa majirani hao
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Yohana Msigwa amesema uongozi wa kata ya
Itundu umeliweka suala la ujenzi wa soko katika mikakati ya kata hivyo
amewataka wananchi kuwa na subira
Amesema kwa sasa wamefyatua tofali 3000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za
walimu wa shule za msingi katika kata hiyo hivyo ujenzi huo ukikamilika
watashughulikia ujenzi wa soko
Naye afisa mtendaji wa kata ya Itundu Bw Isaack Chengula amekiri kuwepo kwa
chagamoto hiyo na kusema kuwa wanasubiri uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu
ukikamilika, watampata diwani ambaye watashirikiana pamoja kutatua chagamoto
hiyo
Amewataka wananchi wa Makusi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki na
utaratibu ukikamilika soko litajengwa
