Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Njombe Mhandisi Julius Subi Akizungumza na mtandao huu juu ya Hofu ya katizo la Umeme Nchini.
Wakati Shirika la Umeme Nchini TANESCO Likitangaza Kuanza Kwa Katizo la Umeme Kwa Muda wa Siku Saba Kuanzia Hii Leo Katika Mikoa Yote Inayotumia Umeme wa Gridi ya Taifa Ukiwemo Mkoa wa Njombe,Hofu ya Hasara na Kukaa Gizani Kwa Siku Zote Imeanza Kutanda Miongoni Mwa Wananchi Mkoani Njombe.
Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Baadhi ya Wafanyabiashara na Wananchi Mbalimbali Mkoani Hapa Juu ya Katizo la Umeme Huo Ambao Unalenga Kuongeza Nguvu ya Nishati Hiyo Kwa Kuanza Kufanya Majaribio ya Umeme wa Gesi ya Mtwara Wamesema Kwa Kipindi Chote Watapa Hasara Kubwa Jambo Ambalo Serikali Inatakiwa Kuangalia Upya Namna ya Kufanikisha Suala Hilo.
Wamesema Kuwa Pamoja na TANESCO Kutaka Kufanya Jambo Lenye Manufaa Kwa Watanzania Wote Lakini ni Vyema Ikaangalia Namna ya Kukata Umeme Huo Hata Kwa Mgao.
Akitolea Ufafanuzi Juu ya Suala Hilo Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Njombe Mhandisi Julius Sabu Amewatoa Hofu Wananchi Hao Kwamba Pamoja na Kuwepo Kwa Taarifa za Katizo la Umeme Huo Kwa Wiki Nzima Lakini Utakuwa Unakatwa Kwa Awamu na Kwa Baadhi ya Maeneo.
na Gabriel Kilamlya