BASATA ladai adhabu kwa Shilole ipo pale pale, yadai inakusanya ushahidi kumtwanga nyundo nyingine

Shilole anaweza akawa anafurahia bata za Marekani baada ya kutumbuiza kwenye show nchini humo, lakini bado BASATA haijamalizana naye.

Katibu Mtendaji wa baraza la sanaa la taifa, BASATA, Geofrey Mngereza ameiambia Radio 5 ya Arusha kuwa adhabu aliyopewa Shilole ya kufungiwa kutojihusisha kwenye masuala ya sanaa kwa mwaka mmoja haijafutwa.

Mngereza alidai kuwa adhabu iliyotolewa kwa Shilole imetokana na sheria na kanuni zilizotokana na bunge na kwamba kwa sasa wanakusanya ushahidi ili kuchukua hatua.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo