Wakazi wa jimbo la mlalo wilayani lushoto wametoa masharti kwa wagombea wa nafasi za ubunge kuwa wanahitaji kiongozi ambaye atakubali kutumika kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusaidia kuwajengea zahanati katika vijiji na shule za sekondari kwa sababu wamechoshwa na ahadi zinazotolewa na wabunge katika chaguzi zilizopita bila utekelezaji wowote.
Wakizungumza katika kata ya Lukozi iliyopo jimbo la Mlalo wilayani Lushoto wakazi hao wamesema wabunge waliochaguliwa katika vipindi vilivyopita wamekuwa wakitoa ahadi nyingi bila ya utekelezaji wowote hivyo wametoa masharti kuwa mbunge ajaye lazima aanze kutatua kero za ukosefu wa kituo cha afya,uchakavu wa barabara na shule za sekondari kuwa mbali ili kuwapunguzia adha wananchi.
Kwa upande wao baadhi ya wagombea kati ya 15 waliojitokeza kuomba ridhaa ya wananchi kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi Bungeni wakijibu masharti hayo baadhi yao wameeendelea kutoa ahadi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa huduma za afya,uchakavu wa barabara pamoja na masoko ya mazao ya mboga mboga ambayo ndio zao kuu la wakazi wa wilaya ya Lushoto.
