TFDA yafunga machinjio ya jiji la Mwanza kwa muda usiojulikana

Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), kanda ya ziwa imeyafunga kwa muda usiojulikana machinjio ya jiji la Mwanza yaliyopo eneo la Nyakato kwa madai ya kukithiri kwa uchafu na miundombinu mibovu na hivyo kusababisha maelfu ya wakazi wa jiji hilo kukosa huduma muhimu ya kitoweo cha nyama.

Meneja wa TFDA kanda ya ziwa Moses Mbambe anasema hii ni mara ya pili kwa machinjio hayo yenye uwezo wa kuchinja ng’ombe zaidi ya 300 kwa siku na mbuzi 200 kufungwa, ambapo mara ya kwanza yalifungwa Novemba 3 mwaka 2014 kwa uchafu.lakini je, ni sababu zipi hasa zilizosabisha TFDA kuamua kuchukua hatua za kuyafunga machinjio hayo.

Kufa kufaana – licha ya machinjio ya Nyakato kutiwa kufuli na mamlaka ya chakula na dawa, sasa neema imemwangukia mmiliki wa machinjio binafsi iliyopo katika eneo la Kisesa ingawa nayo imelalamikiwa kwa kutokidhi viwango vya ubora pamoja na suala la usafi. 
 
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza Tito Mainya amewatoa wasiwasi wakazi wa jijini hapa kuhusiana na kufungwa kwa machinjio hayo, huku baadhi ya walaji wa nyama wakilalamikia hali hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo