Tanzania imepata heshima ya pekee ya uhifadhi na ulinzi wa faru barani arfika baada ya askari wa wanyamapori katika hifadhi ya taifa ya Serengeti koplo Patrick Malale Mwita kushinda tuzo ya mwaka ya askari bora katika ulinzi wa faru afrika inayotolewa kila mwaka.
Askari huyo wa wanyamapori amekabidhiwa tuzo hiyo jijjini Johannesburg Afrika kusini na mwana wa mfalme wa Monaco ambaye ndiye mlezi wa tuzo hiyo ambayo kwa mujibu wa afisa uhusiano wa Tanapa Bwana Pascal Shelutete miongoni mwa vigezo vilivyompa tuzo koplo mwita ni pamoja na umahiri wake wa kutambua asilimia tisini ya faru wote waliopo ndani ya hfadhi ya Serengeti kwa alama.
Akizungumzia ushindi huo koplo Malale Mwita anasema ni heshima kubwa kwa Tanapa na tanzania kutokana na umuhimu wa faru katika kukuza utalii.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Tanapa Bwana Mtango Mtahiko anasema ipo haja kwa watanzania na wadau wote kushiriki kwenye ulinzi wa wanyama waliopo hatarini kutoweka.
Tuzo hizo imekuwa zikiandaliwa kwa lwa ushrikiano baina ya wizara ya mazingira ya afrika kusini na chama cha askari wanyamapori cha Afrika.
