Ratiba ya uchukuaji fomu za kugombea urais,ubunge na udiwani

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imetangaza ratiba ya uchukuwaji fomu za kugombea urais, ubunge na udiwani ambapo zoezi hilo linaanza August mosi huku ikiwatahadharisha wagombea hao kuhakikisha wafuasi wao hawasababishi vurugu vinginevyo sheria itachukuwa mkondo wake.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kila chama na wagombea wao wanakumbushwa kuzingatia maadili ya uchaguzi na kutoa angalizo kwa viongozi wa kisiasa kuwa waangalifu na matamshi yao kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kwamba vyama ambavyo tayari vimeshatoa taarifa tume na kupangiwa tarehe ya kuchukuwa fomu ni UPDP, TLP, DP, CCM, ADC, TADEA na ACT.
 
Katika hatua nyingine jaji Lubuva amepiga marufu vikundi vya vijana wanaowalaghai wananchi na kukusanya kadi zao za kupigia kura kwa madai kuwa watapata mikopo chapuchapu kwani kitendo hicho ni uvunjivu wa sheria na hakuikubaliki na kuhusu taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwatahadharisha watu kutokuhakiki vitambulisho vyao kwa kutumia namba maalu zilizotolewa na tume jaji Lubuva amesema.
 
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ambaye amehudhuria mkutano huo wa waandishi wa habari na tume amesema jeshi la polisi litaongeza askari katika barabara ambazo zitatumiwa na wagombea hao ili kuhakikisha ulinzi unakuwepo wa kutosha na kuwataka wagombea na wafuasi waio wasiwe chanzo cha kusimamisha shughuli za kijamii.
 
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida siku moja baada ya tume ya uchaguzi kuongeza muda wa kujiandikisha baadhi ya vituo vilikuwa havina msongamano wa watu kama ilivyokuwa awali huku vingine waandikishaji wakisubiri watu ambapo pia mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dk Reginald Mengi akiongozana na mkewe Bi Jackline Mengi wamejiandikisha katika kituo cha shule ya msingi ananasifu Kinondoni.
 
Hadi sasa watu zaidi ya milioni mbili wameshaandikishwa jijini Dar es Salaam na kufanya idadi ya watu waliokwishaandikishwa nchi nzima kufikia milioni ishini na moja na sabini elfu. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo