Jinsi Magufuli alivyoibuka kidedea kugombea urais CCM 2015

MBUNGE wa Biharamulo Mashariki (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli ameshinda katika uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 2104 sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali amepata kura 253 sawa na 10.5% na Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ndiye aliyepewa jukumu la kutangaza mshindi aliyepatikana kwa kura za Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi mkoani Dodoma.
KURA ZILIZOPIGWA: 2422
KURA ZILIZOHARIBIKA: 6
KURA HALALI: 2416

Muda mfupi baada ya Dk John Magufuli kutangazwa na chama cha mapinduzi kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea nafasi ya urais amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anawashughulikia wala rushwa na wabadhilifu wa mali za umma kikamilifu.

Ametoa ahadi hiyo katika viwanja vya jamuhuri mjini Dodoma alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara wakati chama chake kilipokuwa kinamtambulisha yeye pamoja na mgombea mwenza ambapo amesema pia atahakikisha wafanyabiashara ndogondogo wanafanyashughuli zao katika mazingira mazuri bila kubughudhiwa.
 
Kwa upande wake mgombea mwenza Mh Samia Hasan Suluhu amesema atahakikisha anashughulikia kero chache zinazoukabili muungano ili kuhakikisha unaimarika na unadumu.
 
Baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma wamepongeza uteuzi huo na kwamba CCM imefanya maamuzi sahihi kwani Dk Magufuli utendaji wake unafahamika na ni imani yao kuwa ana uwezo wa kuwatoa kwenye wimbi la umaskini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo