Aliyembaka mjukuu wake na kumuambukiza UKIMWI awaliza wengi...CCM yatoa neno

Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kitendo cha mkazi wa kijiji cha Nyarombo wilayani Rorya mkoani Mara Isack Okanga aliyekamatwa kwa tuhuma ya kumbaka na kumuambukiza virusi vya ukimwi mjukuu wake mwenye umri wa miaka 12.

Katika ziara ya chama kwenye vijiji vya kata ya Nyamtinga wilayani Rorya, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Samwel Kiboye amewataka wananchi kuwafichua wanaofanya vitendo vya ubakaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Rorya Samwel Kiboye amesema kwamba, kitendo cha mzee Isack Okanga mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa kijiji cha nyarombo wilayani humo cha kumbaka mjuu wake na kumuambukiza virusi vya ukimwi, huku akijua kwamba yeye ni muathirika wa ugonjwa huo kwa mda mrefu nakusema ni kitendo kibaya na cha kikatili na kinapaswa kulaaniwa na kila mmoja wetu
Samwel Kiboye amelipongeza jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kutoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Rorya kuhusu vitendo vya ubakaji na ukatiri dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa uapande wa afisa ustawi katika Hosipitali ya Mennonite, iliyopo Shirati wilayani Rorya, Mecktrida Charles amesema, katika kipindi cha miaka miwili, zaidi ya matukio 100 ya ubakaji kwa watoto wa kike walio na umri  chini ya miaka 18 yamelipotiwa katika ofisi yake.
Samwel Kiboye ametoa kiasi cha shilingi laki mbili kwa mtoto alie bakwa kwa ajiri ya kununua mahitaji ya shule.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo