Wasomi nchini wamekipongeza chama cha mapinduzi CCM kwa kumaliza mchakato wa kumtafuta mgombea wa chama hicho bila kuleta mpasuko wowote wa kiitikadi.
Katika mazungumzo yao kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wamesema kumalizika salama kwa mchakato huo ndani ya CCM ni matokeo ya uongozi imara wa mwenyekiti wa chama hicho rais Jakaya Kikwete, Dkt Ayoub Lioba ni mhadhili wa chuo kikuu cha habari ambaye pia anakiri kuwa CCM imemchagua mgombea imara.
Licha ya mgombea huyo wa CCM kutajwa kukubalika ndani na nje ya CCM, watanzania na wanaccm kwa ujumla wametakiwa kuhakikisha wanakuwa makini na baadhi ya wagombea na kuachana na makundi kwani yanaweza athiri amani ya nchi, kama Prof Mwesiga Baregu mchambuzi wa masuala ya kimataifa anavyozungumza.
Dkt Onesmo Kiauke mhadhili wa sheria UDSM, anasema kupitishwa kwa Dkt John Magufuli itakuwa ni athari kubwa kwa vyama vya upinzani ambavyo hadi sasa vimeshindwa kufikia muafaka wa nani atasimama katika kinyanganyiro cha urais mwaka huu.