na mimi mapanga nayaweza

 
Mwanamuziki aliyeibukia kwenye shindano la Bongo Star Search, Baby Madaha, amejiunga rasmi kwenye Kundi la TMK Wanaume Halisi ambalo linaongozwa na Juma Kassim Ally Kiroboro ‘Sir Nature’.
 
Habari kuwa Baby ni memba wa Halisi, zimethibitishwa na yeye mwenyewe pamoja na kiongozi wa kundi hilo Juma  Nature a.k.a Msitu wa Vina.Staa huyo alipoulizwa alikiri kufanya kazi na Halisi na kuongeza kwamba mwaka huu ameamua kujipanga vyema zaidi ndiyo maana ameungana na vichwa vya kiumeni.
 
Kwa upande wa Nature, alijibu: “Unauliza maembe kibada? Baby Madaha ndiye first lady wa Halisi.
 
Tumemchukua kwa sababu anaweza kazi.”aada ya kumaliza msimu wa BSS, Baby alifanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini alipotoa ngoma yake inayokwenda kwa jina la Amore, ilimtambulisha vema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo