CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya mapingamizi yake 155 kwa wagombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jiji la Arusha kutupwa.
Mapingamizi
hayo yaliwasilishwa kwa Katibu Tawala wilaya ya Arusha na msimamizi
mkuu wa uchaguzi, Juma Iddy ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha
kwa ajili ya kusikiliza rufaa.
Akitoa
uamuzi huo juzi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Daniel Machunda
alisema mapingamizi yaliyowasilishwa na Chadema, yalidai kuwa wagombea
wa CCM walikuwa hawajadhaminiwa na chama chao.
Machunda
alisema mbali na hilo, mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa Novemba 23
mwaka huu na mapingamizi yote yalitakiwa kuwasilishwa ndani ya siku
mbili kuanzia Novemba 24, lakini Chadema waliyawasilisha Novemba 26,
hivyo kuwa nje ya muda uliopo kikanuni.
“Kwa
mujibu wa kanuni ya uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati
ya mtaa katika mamlaka za mji za mwaka 2014 (15) (2) kinasema;
“Pingamizi chini ya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii itawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi ndani ya siku mbili tangu kufanyika kwa uteuzi na msimamizi atatoa uamuzi kwa muda usizidi siku mbili kwa kuanzia siku aliyopokea pingamizi hilo’’ alisema.
“Pingamizi chini ya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii itawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi ndani ya siku mbili tangu kufanyika kwa uteuzi na msimamizi atatoa uamuzi kwa muda usizidi siku mbili kwa kuanzia siku aliyopokea pingamizi hilo’’ alisema.
Alisema
kwa mujibu wa kanuni hiyo mapingamizi yote ya Chadema yaliyowasilishwa
Novemba 26 mwaka huu yalipelekwa nje ya muda na kwa mantiki hiyo
pingamizi hizo yametupiliwa mbali.
Akizungumzia
hali hiyo, Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz Juma alisema
amefurahishwa na uamuzi huo. Mapingamizi hayo yaliwalenga wanaCCM
wanaowania uongozi katika Kata za Kaloleni, Unga Ltd, Ngarenaro, Olerien
na Levolosi.