Godawn la Kampuni ya Simba Mtoto lilolopo eneo la Tabata Matumbi
jijini Dar es salaam, limenusurika kuteketea kwa moto usiku huu, baada
ya vijana wawili waliokuwa wakiishi katika eneo lilolopo jirani na hapo,
kuchoma matairi mabovu yaliyokuwepo ndani ya eneo lao hilo.
Walipoulizwa sababu za wao kufanya hivyo, vijana hao waliofahamika kwa
majina ya Peter na Amdan, wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi, walisema
kuwa walifanya hivyo kwa lengo la kupunguza wingi wa majani
yaliyolizunguka eneo hilo na hawakuwaza kama moto huo ungeshika kwenye
matairi hayo ambayo ni chakavu ya magari yaliyokuwamo ndani ya eneo
hilo.
Taharuki ilitanda eneo lote la Tabata pale moshi mwingi na mzito
ulipotanda angani na kuwafanya hata wale waliokuwa kwenye mapumziko ya
mwisho wa wiki kushindwa kufanya hivyo huku wengine wakifanya
mawasiliano na baadhi ya ndugu zao waliowaacha majumbani.
Hadi Ripota
wetu anaingia mitamboni hakukuwa na madhara yeyote yaliyotokea na
jitihada za kukitafuta kikosi cha Zimamoto na Uokoaji zilikuwa
zikiendelea.
Na vijana hao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka.
vijana hao ambao walifahamika kwa jina Moja Moja, Peter na Amdan wakipakizwa kwenye gari ya Polisi.
Vijana hao wakiwa chini ya Ulinzi. chanzo michuzi blog