LOWASSA AZIDI KUPETA NDANI YA CCM, UTAFITI MWINGINE UMEONESHA HIVIIIIII................!!!!!!

Kwa mara ya pili jina la Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa limetajwa kwenye ripoti ya kitengo cha utafiti cha jarida la Economist Intelligence Unit EIU kuwa ndiye mwanasiasa anayekubalika zaidi ndani ya CCM kuwania Urais mwakani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya EIU yenye makao yake makuu London,Uningereza ilitolewa December 19 mwaka huu na ushindani unaoendelea kwa sasa baina ya wanasiasa sita wanaodaiwa kuendesha kampeni za kuwania urais mwakani utakigawa Chama hicho,lakini hautakinyima ushindi.

Makada wa CCM wanaodaiwa kuwania kiti cha Jakaya Kikwete ni pamoja na Lowassa,Waziri mkuu Pinda,Fredrick Sumaye,Willium Ngeleja,Bernad Membe,Steven Wassira na January Makamba.

Ukimuacha Pinda makada waliosalia katika orodha hii wamekwishatiwa hatiani na kamati kuu ya CCM kwa kuendesha kampeni za kuwanaia nafasi hiyo kinyume na sheria jambo ambalo limezua mgawanyiko wa kimakundi na kuhatarisha umoja ndani ya Chama hicho.

“CCM itagawanyika katika kumpata mshindi wa kiti cha urais,nakundi la Waziri mkuu wa zamani Lowassa ndilo linaloonekana kuwa na nguvu kubwa ya mgombea wake kuteuliwa kuwania Urais,,,hata hivyo Pinda anafanya vizuri na sasa kundi lake ndilo linaloshika nafasi ya pili nyuma ya lile la Lowassa”lilieleza jarida hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo