UMEIPATA HII.................MAITI ZAIHIFADHIWA KWENYE KORIDO YA HOSPITALI HUKO GEITA

Hospitali ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita ina tatizo kubwa na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti hali inayosababisha zihifadhiwe kwenye korido.

Hali hiyo ilibainika baada ya mwalimu wa shule ya Msingi Kasandalala Wilayani humo Laideth Constantine mwenye miaka 33 kuthibitika kuwa alimnyonga mtoto wa miaka saba na maiti yake kuhifadhiwa kwenye korido.

Kutokana na tukio hilo Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Cosmas Kilosa alisema hospitali hiyo ina changamoto kubwa ya kukosa sehemu ya kutunza maiti hali iliyosababisha maiti hiyo kuhifadhiwa kwenye korido.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo alisema mwalimu huyo anashikiliwa na Polisi baada ya vipimo vya daktari kuthibitisha kuwa mtoto huyo kanyongwa.

Alisema mwili wa marehemu ulikua umejaa damu nyeusi,uvimbe pamoja na kutokwa na ulimi mrefu nje na inasemekana mwalimu huyo ndiye aliyehusika na tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo