Katika hali isiyoua ya kawaida wanaume watatu,wawili wakazi wa
jijini Mwanza walizua tafrani baada ya kung’ang’nia maiti ya Happy
Wangoge Mathias mwenye umri wa miaka 33 aliyekufa siku chache baada ya
kufunga ndoa na Pascal Mayalla.
Hiyo inatajwa ilikua ndoa ya tatu ya marehemu huyo anayedaiwa alikua
ni mke wa mtu na kwamba aliolewa na mahari ya ng’ombe 11 na mwanaume
Chanjo Ryoba mkazi wa Nyamongo Wilayani Tarime aliyezaa naye mtoto
mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 14.
Tukio la kuing’angania maiti hiyo lilianza rasmi jumamosi iliyopita
baada ya mke huyo kufariki dunia ambapo inasemekana enzi za uhai
wake,Happy alikua akiishia Jijini Mwanza na ujihusisha na biashara ya
samaki na aliolewa tena na Benjamini Bushoti kabla ya hivi karibuni
kufunga ndoa ya kikristo na Mayalla.
Aliyeanzisha vurugu hizo ni mumewe wa pili ambaye alikua akiishi naye
na alizaa naye watoto wawili kabla ya kufunga ndoa na Mayalla ambapo
uvumilivu ulimshinda baada ya kuwaeleza waombolezaji yeye ndiye mume
halali wa marehemu na alikua akiishi naye pamoja na watoto wao wawili.
Kufuatia tukio hilo watu mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa mtaa
walimtuliza mume huyo wakimsihi aache vurugu ili waangalie hoja iliyokua
mbele ya kuandaa safari ya mwisho ya kwenda kumzika marehemu.