Mtoto mlemavu wa akili na miguu mwenye miaka14 anadaiwa kubakwa na
kuambukizwa magonjwa ya zinaa na mwanaume mwenye umri wa miaka50.
Mwanaume huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho siku moja kabla ya
kufunga ndoa na mke mpya aliyemlipia mahari eneo la Uyole Mbeya baada ya
kuachana na mke wake wa kwanza aliyezaa naye watoto zaidi ya watatu.
Tukio hilo lilitokea November 4 na kuripotiwa kituo cha polisi ambapo
mpaka sasa mtuhumiwa anasakwa na polisi kwa ajili ya ufunguliwa kesi ya
kubaka.
Shangazi wa mtoto huyo akizungumza kwa masikitiko alisema waligundua
mtoto wao amefanyiwa kitendo hicho baada ya kutoka kwenye nyumba ya
mtuhumiwa huyo huku akilia na walipomchunguza ndipo walipobaini kuwa
amebakwa na vipimo vilionyesha ameambukizwa magonjwa ya zinaa.