Zaidi ya wanafunzi 100 wa Shule ya Msingi Hananasif na Mkunguni za
Wilayani Kinondoni,Dar es salaam wanadaiwa kulawitiwa na wanaume kwa
nyakati tofauti.
Taarifa zilieleza kuwa wanafunzi hao wa darasa la kwanza hadi la nne
wanaosoma madarasa tofauti wanafanyiwa vitendo hivyo nje ya shule na
maeneo wanayotoka.
Kutokana na taarifa baadhi ya wazazi na hata taasisi za Serikali na
uongozi wa shule ya Hananasifulilazimika kuitisha vikao vya dharura
kujadili suala hilo.
Chanzo cha kuaminika kutoka ,shuleni hapo kilidai mwalimu mkuu hiyo
aliwaita wanafunzi kadhaa na kuwahoji na baadhi yao walikiri na kuw
ataja wnaaume wanaowafanyia vitendo hivyo na mahali wanapofanyia.
Baadhi ya wanafunzi hao walisema aliwahi kufanyiwa kitendo hicho
nyumbani kwao na alishahojiwa na mwalimu wake mkuu na kumweleza ukweli
huku mwanafunzi mwingine wa kiume wa darasa la pili alidai huwa
anafanyiwa na kijana mmoja ambaye humpa vitumbua.
“Mimi nilifanyiwa muda kidogo, nimesahau siku,wakati narudi nyumbani
nilikutana na mtu kichochoroni akanifanyia hivyo lakini nilimwambia mama
na akanimabia nikatoe taarifa kituo cha polisi