Polisi kanda ya Dar es salaam wametoa tahadhari kwa wanawake kuacha kushiriki mapenzi na watu wasiowafahamu ili kuepuka kuuawa.
Taarifa ya Kamishna wa Kanda Suleiman Kova ilisema wasichana hususani
wa jijini Dae es salaam wanatakiwa kuwa makini na wanaume wasiowajua
kwa sababu wengi wameishia kuuawa kikatili huku miili yao ikitelekezwa
hovyo.
“Kuna taarifa ya kuwepo wanaume wawili
wanaowashawishi wanawake kufanya nao mapenzi na baada ya muda
huwaua,natoa tahadhari kwa wanawake wote kuwa makini na watu
hawa”alisema Kova.
Alisema siku za hivi karibuni kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji
ya aina hiyo ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wameshapoteza
maisha.