KIJANA mmoja wa kiume
aliyedaiwa kuwa ni mfanyabiashara ndogondogo amekutwa amefariki katika
kituo cha mabasi yaendayo kasi Manzese, jijini Dar, leo asubuhi.
Inasemekana vijana wengi huwa wana tabia ya kulala ndani ya vituo hivyo
kwa hiyo watu iliwachukua muda mrefu kubaini kama amefariki.
Kwa mujibu wa mtendaji wa serikali wa
Kata ya Midizini-Manzese, Penford Kizo, wa eneo hilo na mashuhuda
wengine, kifo cha kijana huyo hakijafahamika kimesababishwa na nini.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI:-
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI:-
(Picha / Habari: Gabriel Ng’osha na Mussa Mateja / GPL)