Mwakilishi
wa Rais wa China, Hon. Chen Changzhi akipeana mkono na mmoja wa
madaktari wakuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo mara baada ya kuwasili
kwenye uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na madaktari kabla ya uzinduzi.
Wawakilishi wa Serikali ya China na Rais Jakaya wakiwa wamesimama kwa heshima wakiimba nyimbo za taifa za nchi hizo.
Waziri wa Afya, Seif Rashid akitoa hotuba fupi.

Rais Kikwete akitoa vyeti kwa wakuu na waliofanikisha uwepo wa idara hiyo.
Rais Kikwete akitoa hutuba fupi ya utangulizi.
Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya JK.
Rais Jakaya na mwakilishi wa Rais wa China Hon. Chen Changzhi wakikata utepe.
Kikundi cha ngoma za asili cha polisi kikitumbuiza kwa ngoma ya kibati.
Rais Kikwete, wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa kitengo hicho katikapicha ya pamoja.
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo amezindua rasmi kitengo cha upasuaji,
tiba na mafunzo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ‘Cardiac Surgery,
Treatment and Training Centre.’
Uzinduzi huo uliokuwa na ugeni wa Mwakilishi wa Rais wa Jamhuri ya
Watu wa China, Hon. Chen Changzhi ambaye serikali yake kwa kushirikiana
na serikali ya Tanzania, wamefanikisha kujenga kitengo hicho nyeti
nchini ili kuondoa tatizo sugu la magonjwa ya moyo nchini.
(PICHA: CHANDE ABDALLAH/GPL)