Tunawafunza nini watoto wetu..?
Leo nimesikitishwa sana na hivi vitendo vya kucheza vibaya mbele za watu....hapa nilikua nipo kwenye foleni morogoro road...hichi kikundi cha watu walikua wanapita huku wakicheza vibaya sijui ndo mdundiko or kigodoro...kibaya zaidi ni barabarani wadada wanacheza mpaka wanatamani wacheze bila nguo...sasa hapo ni mchana kwenye mwanga usiku je si inakua zaidi..?
Tunataka tupewe heshima je hiyo heshima tutaipata kimtindo huu...?Tunaenda wapi wajameni....tunawafunza nini watoto wetu....?
KUTOKA KWA MDAU JOYCE KIRIA
