LIVERPOOL HOI KWA CHELSEA, YAPIGWA MABAO 2-0

Demba Ba akiifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 45 ya mchezo.
Chelsea wakishangila bao lao la kwanza.
Liverpool hoi baada ya kipigo.
Willian akiifungia Chelsea bao la pili dakika ya 90.
 
Ba na Sakho wakichuana.

TIMU ya Liverpool imepokea kipondo cha bao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Uwanja wa Anfield jijini Liverpool leo.

Mabao ya Chelsea yamewekwa kimiani na Demba Ba dakika ya 45 wakati la pili likifungwa na Willian dakika ya 90.

Kwa matokeo ya leo, Chelsea wamefikisha pointi 78 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 36 wakati Liverpool wakibaki kileleni na pointi 80 wote wakisalia na mechi mbili kumaliza ligi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo