WAZIRI mpya katika Wizara ya Maliasili
na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu na Naibu Waziri mpya mh. Mahmood Mgimwa
wamepokelewa kwa shangwe mapema Jana makao makuu ya wizara ya Maliasili
na Utalii jijini Dar es Salaam.
Wizara
ya Maliasili na Utalii imefanya mapokezi ya Mawaziri wake wapya leo
Jumanne 21 Januari 2014, ambapo watumishi waliopo Makao Makuu ya wizara
wamepata fursa ya kukutana na kufanya maongezi na mawaziri hao.
Mapokezi hayo yanafuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzanaia Mhe. Jakaya Kikwete.
Naibu
Waziri Mhe. Mahmood Mgimwa amewaahidi wafanyakazi wa Maliasili na
Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kuleta
maendeleo ambayo wananchi wanayategemea kutoka katika Wizara hii.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na
Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewakikishia wafanyakazi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kuweza
kuifanya Wizara kuongeza pato la Taifa kupitia Utalii.
Aidha,
Mhe Nyalandu amewaasa watumishi wote kudumisha amani na upendo katika
maeneo yao ya kazi ili kujenga mazingira mazuri ya kazi na kuongeza
ufanisi..
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. M.Tarishi (kushoto), Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa (Katikati) na Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Kulia) wakibadilishana
mawazo baada ya mkutano wao na watumishi wa wizara ya maliasili na
utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akiongea na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akisalimiana na
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Kidegesho.



