Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dkt. Wilbroad Slaa wanatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya mabehewani Makete mjini alhamisi ya wiki hii kwa lengo la kukiimarisha chama chao
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Makete Shaaban Mkakanze amesema lengo la ziara hiyo ni kuzungumza na wananchi hivyo kuwaomba wanamakete wote bila kujali itikadi zao za vyama kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo
Mkakanze amesema viongozi hao watawasili kwa helkopta wilayani Makete alhamisi ya wiki hii majira ya saa tao asubuhi ambapo pia watasindikizwa na viongozi wengine wa chama hicho
"Kama mnavyojua CHADEMA ni chama cha wananchi hivyo inafaa wananchi mkajitokeza kwa wingi bila kujali ukabila, dini, rangi ama unatoka chama gani ila cha msingi kata zote 22 za wilaya hii zijitokeze kwa wingi kuwasikiliza viongozi hao wanawaambia nini" alisema Mkakanze
Mara baada ya viongozi hao kumaliza mkutano huo wilayani Makete wataelekea wilayani Kyela mkoani Mbeya kuendelea na ziara yao