Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita (Kushoto)
akiteta jambo na Mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Kiboriloni wa
tiketi ya chama cha Mapinduzi, Willy Adriano, wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo kuziba pengo lililoachwa wazi na
aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata hiyo,, Marehemu Vincent Rimoy
aliyefariki dunia Novemba 6, mwaka jana.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanajro, Iddi Juma,
(aliyeshika kipaza sauti), akimnadi mgombea wa CCm katika Uchaguzi
mdogo wa Udiwani, Wlly Adriano katika uchaguzi uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo
lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwanbi wa Kata ya
Kiborloni, Vincent Rimoy, alyefariki dunia ghafla Novemba 6 mwaka
jana.
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi (kushoto), akiwa
akimtambulisha Mgombea wa Udiwani katika kata ya Kiboriloni, Willy
Adriano aliyesimama katikati, kulia kwake ni Mke wake.(Picha zote na
Taifa Letu.com Blog)
akimtambulisha Mgombea wa Udiwani katika kata ya Kiboriloni, Willy
Adriano aliyesimama katikati, kulia kwake ni Mke wake.(Picha zote na
Taifa Letu.com Blog)
========= ======= =========
Na Mwandishi Wetu, Moshi
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), mwishoni mwa wiki walifanya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kiboriloni liliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Vincent Rimoy (CHADEMA), aliyefariki ghafla Novemba 6 mwaka jana.
Wa kwanza kufanya uzinduzi ni Chadema, waliozindua kampeni yao kwa
mbwembwe wakimtambulisha mgombea wao, Frank Kagoma ambaye ni
mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi, uzinduzi ulioongozwa na viongozi
mbalimbali wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani hapa akiwemo
mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemon Ndesamburo.
Wakizungumza katika Nyakati tofauti katika uzinduzi huo uliofanyika,
Jumamosi ya Januari 18, mwaka huu, katika stendi ya kidia, viongozi wa
Chadema walianza kumnadi mgombea wao ambap[o walimtaja kama mtu sahihi ambaye anaweza kuendeleza mapambano ya chama hicho ndani ya baraza la madiwani kupinga ufisadi na uonevu katika manispaa ya Moshi.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, aliwataka wananchi wa kata
hiyo kumchagua mgombea wa Chadema kwani ndiye mwenye uwezo wa
kutekeleza yale yote aliyoyaanzisha Marehemu Rimoy ndani ya kata hiyo
na baraza la madiwani.