Mahmoud Ahmad Arusha
Mkutano
wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa
kwamba Ziwa Manyara (pichani) lipo hatari ya kutoweka kabisa kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa mazingira unakotokana na Kilimo
pembezoni mwa mito kama juhudi za makusudi hazikuchulia kutunza
mazingira yanayozunguka maeneo ya mito mbalimbali inayoingia ziwani
humo.
Hali
hii imetokana na kuongezeka kwa shughuli za kibianadamu hussani za
kiuchumi na kusababisha pia Ziwa Manyara kujaa udongo na matope pamoja
uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akiwasilisha
mada kuhusu changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa
Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bi. Christina Kiwanga amesema
kukosekana kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa
ziwa hilo.
Bibi
Kiwanga ametaja changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa mipango
endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu umuhimu wa uhifadhi sanjari na
elimu.
Muikolojia
huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha kwamba
shughuli za Biandamu hususani za Kilimo na za kiuchumi zimechangia kwa
kiwango kikubwa hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.
Naye
Meneja Ujirani Mwema makao makuu ya TANAPA Bw. Ahmed Mbugi amesema
umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama
katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shoroba zilizokuwepo miaka ya
nyuma zimetoweka kabisa.
Amesisitiza kwamba ni lazima wananchi walinde uasilia wa mapito ya wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo
Mbungi
amefafanua kwamba awali kulikuwa na Maeneo ya SHOROBA yenye ukubwa wa
ekari 40,000 katika hifadhi za Arusha Kilimanjaro, Manyara lakini
maeneo haya yamepungua.
Aidha
amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia kuhujumu maeneo haya ya
uhifadhi kutokana na kukosekana kwa kuchukuwa maamuzi mazito ya
kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta changamoto
mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.
Pia
ameeleza kwamba asilimia 70 ya mapato yanayotokana na uhifadhi
yanatumika katika kusajidia utekelezaji wa miradi ya kijamii ikiwemo
ya Afya,Elimu, Maji, na miradi ya Barabara.
Amesema
migongano baina ya wanyamapori na binadamu inachangiwa na binadamu
kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za
kupita hali inayoharibu mazingira.
Amesisitiza
kwamba hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za utalii ambapo idadi
ya watalii hupungua sanjari na shughuli za Uchumi kuathirika Mbali na
hali hii katika kipindi cha mwaka 1957/63 na 1987/`988 uoto wa
asilimia hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5 wakati maeneo ya
kilimo yaliongezeka kwa asilimia 10.9.
Aidha
maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa shughuli za kilimo kati ya mwaka
1997/98 yaliongezeka kati ya asilimia 8.35 hadi 11.41.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye
amesema kasi ya ziwa mmnyara kuendelea kujaa ugondo na matope ni ya
kasi zaidi.