WANANCHI KIJIJI CHA LIMAGE KATA YA YAKOBI NJOMBE WAMEANZA KUPATA MAJI YA BOMBA TANGU NCHI HII IPATE UHURU

Na   Gabriel Kilamlya Njombe

Hatimaye Wananchi wa Kijiji Cha Limage Wilayani Njombe Wameondokana na Tatizo la Huduma ya Maji Safi na Salama Lililokuiwa Linawakabili Kwa Muda Mrefu Baada ya Wananchi Hao Kuanza Kupata Huduma ya Maji ya Bomba.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Limage Emmanuel Mtedzi Amesema Kuwa Huduma ya Maji Kwa Sasa Inapatikana Kwa Takribani Asilimia 80 Licha ya Mradi Huo Kutokamilika Kwa Asilimia Mia Moja.

Amesema Kuwa Licha ya Mradi Huo Kuanza Kutumika Lakini Bado Kunahitajika Zaidi ya Shilingi 271 Kwa Ajili ya Kukamilisha Mradi Huo Ambapo Ulitakiwa Kukabidhiwa Kwa Wananchi Mwezi Uliopita.

Aidha BwanaMtedzi Ameongeza Kuwa Kukamilika Kwa Mradi Huo Utawanufaisha Wakazi 1943 wa
Kijiji Hicho na Maeneo ya Jirani Waliokuwa Wakisafiri Umbali Mrefu Kwa Ajili ya Kupata Huduma ya Maji Safi na Salama.

Akielezea Baadhi ya Changamoto Zinazojitokeza Mwenyekiti Huyo Amesema ni Pamoja na Uharibifu Unaofanywa na Baadhi ya Wananchi na Watoto Ambao Wanakata Mabomba Huku Akiwataka Wananchi Kuitunza Miundombinu ya Maji.

Upatikanaji wa Huduma ya Maji Imetokana na  Jitihada za Michango ya Wananchi Kwa Kushirikiana na Halmashauri  ya Mji wa Njombe Ambapo Machi 18 Mwaka Huu Wakati wa Wiki ya Maji Diwani wa Kata ya Yakobi Bi.Ester Mgeni Aliweka Jiwe la Msingi Katika Mradi Huo wa Maji


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo