skip to main |
skip to sidebar
MKE MWENZA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MAKETE KWA TUHUMA ZA KUMMWAGIA MAJI MOTO MKE MWENZAKE NA KUMJERUHI VIBAYA

Jeshi
la polisi wilayani Makete mkoa wa Njombe linamshikilia Bi Rose Skwea Tweve mkazi wa
kijiji cha Isapulano kwa tuhuma za kummwagia maji ya moto mke mwenzake
Estina Kristian Sanga [23] pamoja na mtoto wake mdogo ambao wamelazwa
katika hospitali ya wilaya ya Makete kwa matibabu zaidi.
akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mrakibu wa polisi ambaye pia ni afisa upelelezi (OCCID) wilaya
ya makete Gosbert Komba amesema matukio ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakijirudia mara kwa mara wilayani hapo huku akiwataka wananchi kufuata sheria na taratibu za nchi.
kwa upende wake Bi Estina Sanga Ambaye amejeruhiwa na mke mwezake huyo
amesema kuwa tukio hilo lilimpata majira ya saa mbili usiku alipokuwa
anakwenda kumjulia hali mume ambae ni mgonjwa nyumbani kwa Bi Rose
ambaye ni Bi mkubwa.
Naye mtuhumiwa wa tukio hilo Bi Rose Tweve
amesema alifikia hatua hiyo baada ya kurushiana maneno na mke mweziye
huyo na kuchukizwa kwa kitendo cha kwenda kumuona mume wao huku akiwa
amelewa ndipo akachua sheria mkononi kwa kumwangia maji ya moto ka njia ya kumuonya.
akizungumzia tukio hilo Bwana Itiso Chaula (32) ambaye ni mume wa wanawake
hao mkazi wa kijiji cha Isapulano amesema ameshangazwa na tukio ambalo Bi
mkubwa amelifanya kwa Bi mdogo na kulaani kitendo hicho.
Occid Komba amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea, lakini amesema kwa taarifa alizonazo majeruhi anaendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa na maji moto usoni na maeneo ya kifuani
Na Aldo sanga
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi