MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA MKOANI NJOMBE

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linamshikilia Maulid Mwalugoya  Mwenye Umri wa Miaka 22 Mkazi wa Mtaa wa Matalawe Mjini Njombe Kwa Tuhuma za Kusababisha Kifo cha William Mtokoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Oktoba 23 Majira ya Saa Nne Kasorobo Asubuhi Eneo la Mtaa wa CCM Mjini Njombe.

ACP Ngonyani Amesema   Tukio Hilo Limetokana na Ugomvi wa Kugombea Chepe Kati ya Marehemu na Mtuhumiwa Wakati Wakifanya Kazi Ambapo Mtuhumiwa

Maulid Mwalugoya Alimkata Marehemu William Mtokoma Sehemu za Kichwani .Katika Tukio Lingine Kamanda Ngonyani Amesema Mtu Mmoja Ambaye

Hakufamika Jina Lake Anaekadiliwa Kuwa na
Umri wa Miaka 28 wajinsia ya kiume Amekutwa Amefariki Huku  Mikono Yake Ikiwa Imefungwa Kamba na Mwili Wake Kutupwa Ndani ya Mto Ruhuji. 

ACP Ngonyani Amesema Mtu huyo Inasadikika Kuwa Ameuwawa na Watu Wasiofahamika na Kuongeza Kuwa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Linaendelea na Uchunguzi Dhidi ya Matukio Hayo.


kwa Hisani ya Michaelngilangwablog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo