Na Gabriel Kilamlya Njombe
Halmashauri ya Mji wa Njombe Imesema
Kuwa Ifikapo Oktoba 28 Mwaka Huu Siku ya Juma Tatu Inaanza Kutekeleza
Agizo la Kuyakamata Malori na Magari yote Ya Mizigo Yaliyoshindwa Kutii
Agizo la Serikali la Kuhamia Kwenye Maegesho yake Kwa Mujibu wa Tangazo
la Serikali Lilitolewa Hivi Karibuni.
Akizungumza na Kituo Hiki Kufuatia Kushindwa Kutekelezwa Kwa Agizo Hilo Lililowataka Wahusika wa Malori Yote Kuhamia Kwenye Maegesho yake Eneo la Sido Karibu na Ofisi za Ujenzi Mjini Njombe Kaimu Mwanansheria wa Halamshauri ya Mji wa Njombe Bwana Bahati Kikoti Amesema Kuwa Kwa Kwa Yeyote Anayekaidi Agizo Hilo Hatua za Kisheria Zitaanza Kuchukuliwa Kuanzia Oktoba 28 Mwaka Huu.
Aidha Bwana Kikoti Amesema Lengo la Kuyahamisha Malori Hayo Sio Kunyanyasa Wafanyabiashara Hao Lakini ni Kutaka Kuokoa Uharibifu wa Miundombinu Ya Barabara Pamoja na Kuepusha Ajali Zisizo za Lazima Kutokana na Kuwepo kwa Malori Hayo Pembezoni Mwa Barabara.
Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Utekelezaji wa Agizo Ulitakiwa Kuanza Tangu Mwisho wa Tangazo Lililotolewa na Halmashauri ya Mji wa Njombe Ambapo Ilikuwa ni Oktoba 14 Mwaka Huu Lakini Kutokana na Ugeni wa Kitaifa wa Rais Kikwete Mkoani Njombe Ulipelekea Kuchelewa Kutekelezwa Kwa Agizo Hilo.
Hata Hivyo Ameeleza Kuwa Kwa Mujibu wa Sheria za Maegesho Zilizotungwa na Wananchi Wenyewe Kila Atakaye Kamatwa na Kosa Hilo Faini Yake ni Shilingi Elfu 50 Huku Akisisitiza Kuwa Wahusika si Wa Malori Pekee Bali ni Wale Wote Wenye Magari ya Kubeba Mizigo.