Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
barabara ya lami ambayo inamaliziwa kujengwa yenye urefu wa mita 600
iliyopo katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Barabara
hiyo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa
ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya
maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (aliyevaa miwani) akiwa na Diwani wa Kata
ya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma, Joseph
Fuime (kulia kwa Dk Nchimbi) wakipita kwa furaha barabara aliyoizindua
Dk Nchimbi mjini Songea mkoani mjini Songea leo. Barabara hiyo yenye
kiwango cha lami ina urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya
Mateka. Dk Nchimbi pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya
sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Sehemu
ya mamia ya wananchi wa Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea wakiwa tayari
kwa kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Dk Nchimbi baada
ya kuzindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600
ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la
msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika ziara yake ya
siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya
sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Dereva
wa bodaboda (pikpiki) akinyanyuliwa juu kwa furaha na wananchi
waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini
(CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi baada ya Mbunge wao kuyajibu maswali yake. Mamia ya wananchi
waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Mjini, Manispaa ya
Songea walipewa nafasi ya kumuuliza mbunge wao maswali mbalimbali. Dk
Nchimbi baada ya kuzindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa
mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia mbunge huyo
aliweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika
ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi
wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akilifungua jiwe la msingi la ujenzi wa
Ofisi ya Kata ya Mateka iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi
pia alizindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600
ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni iliyopo katika Kata ya Mjini,
Manispaa ya Songea. Dk Nchimbi yupo mjini Songea katika ziara ya siku
tano ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata
ya Mateka, Mjini Songea baada ya kuizindua barabara yenye kiwango cha
lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni
iliyopo katika Kata ya Mjini na baadaye kuweka jiwe la msingi katika
ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika ziara yake ya siku tano
jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari
pamoja na nyumba za walimu.