FILAMU YA MAREHEMU SHARO MILLIONEA AKIWA MDOGO HII HAPA

Hussein Mkieti
Marehemu Sharomilionea mwigizaji wa Filamu Swahiliwood.

SHAROMILIONEA, ambaye kwa sasa ni marehemu aliyefariki kwa ajali ya gari akielekea kijijini kwao lusanga, alionyesha umahiri mkubwa wa uigizaji muda mrefu kupitia filamu ya Safari ya Adili filamu iliyoigzwa kwa umahiri mkubwa na kuwashirikisha wasanii wenye uwezo akiwemo marehemu Sharomilinea, ambaye kwa kiwango fulani kama alitabiri kifo chake.

Sharo akitumia jina la Mkieti alijikuta akimtamani Jini na kupanga kuoana na jini Siti baada ya mtoto wa mfalme, Sharo kukubaliwa kumuoa jini alipewa sharti la kufa ndipo amuoe Siti na kweli sharo alifariki katika filamu hiyo na kuishi na jini, kuna maneno alkiyaongea yanatia simanzi.


Hussein Mkieti
Sharo akiwa na waigizaji wenzake location.
Hussein Mkiety
Sharo sehemu aliyoigiza kafariki ktk filamu ya Safari ya Adil.

Katika filamu ya Safari ya Adili Sharo kaigiza kama mganga wa kienyeji ambaye alitimua mbio baada ya kuona waganga wenzake wakiuawa baada ya kushindwa kumtibia mke wa Mfalme aliyekuwa mgonjwa sana Sharo akiwa polini kajificha anakutana na kundi la mtoto wa mfalme Adil anayesafiri safari ya mbali kutafuta dawa ya mama yake akiwa na walinzi wa mfalme.

Mtayarishaji wa filamu ya Adil Gumbo K anasema kuwa filamu hiyo ilichelewa kutoka kwa sababu alikuwepo nje kwa masomo hata alivyorudi alisikitika kwa kifo cha Sharo kilichomsikitisha ndipo rafiki yake Bendera alipomuomba aitoe filamu hiyo kwa jamii na kubaini filamu ya kwanza kabisa ya Sharomilionea kuigiza akiwa bado mdogo sana.
Hussein Mkiety na Siti
Sharomilionea akiwa na Binti Siti aliyeigiza kama jini.
Hussein Mkiety
Sharo akiwa katika pozi.
Filamu ya Safari ya Adil inatarajia kutoka hivi karibuni na kusambazwa nchi nzima Wapenzi wa filamu wajiandae kumuona Sharomilionea katika filamu ya kiasili kazi iliyo bora, wengi wanamjua Sharo kupitia komedi zilimpa jina kutoka na staili yake ya Oooh mamaa!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo