FILAMU ya mwisho kuigizwa na msanii nguli wa filamu Swahiliwood marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ iliyopewa jina la Love and Power inatarajia kuzinduliwa kwa aina yake baada ya wasanii kutoka Afrika magharibi kuarikwa kwa ajili ya tukio hilo la kuingia sokoni filamu ya mwisho ambayo wengi wanaisubiri kwa hamu ili waone kazi hiyo.
.
Akiongea na FC mratibu wa tukio hilo Mosses Mwanyilu amesema kuwa
msanii huyo alikuwa ni kipenzi cha wapenda filamu Bongo na nje ya mipaka
ya Bongo kwa kuliona hilo wameamua kuarika wasanii mbalimbali kwa ajili
ya kuzindua filamu hiyo ambayo inasemekana kuwa ni kazi ya kipekee.
“Tunatarajia kufanya tukio la kipekee kabisa katika uzinduzi wa
filamu ya Love and Power ya marehemu Kanumba kwa sababu ni mtu wa watu
kwa hiyo kutokana na habari tumekuwa tukizipata kutoka sehemu mbalimbali
kuna watu ambao bado hawaamini kuwa Kanumba yupo hai, katika kumuenzi
tumekusudia kuitendea haki filamu yake,”anasema Mwanyilu.
Filamu ya Love and Power ni filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu na
wapenzi wa filamu kutokana na kile kilichowahi kusikika kuwa filamu hiyo
ilitabri kifo cha marehemu Kanumba, katika filamu hiyo pia wapo wasanii
kama Irene Paul, Patcho Mwamba, marehemu Sharomilionea na wasanii
wengine wengi
CHANZO:FILAMU CENTRAL