Zaidi ya
kiasi cha shilingi milioni 21.658 zimefanikiwa kukusanywa za mfuko wa elimu kwa
mwaka jana ambazo zimetumika kuinua elimu katika kata ya Endiamtu iliyopo
Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara
Taarifa hiyo
imetolewa na Ofisa mtendaji wa kata
hiyo,Edmund Tibiita wakati akiongea kwenye kikao cha maendeleo cha
kata hiyo (WDC) ambapo alieleza kuwa fedha hizo zilichangwa na
wananchi mbalimbali wa vitongoji vinne vinavyounda kata hiyo.
Aidha
alisema kuwa kitongoji cha
Kazamoyo walichanga shilingi milioni 8.3 ,Zaire walichanga shilingi milioni
2.7,Kairo walichanga shilingi 750,000,kitongoji cha Sekondari walichanga
shilingi milioni 2 na kitongoji cha Kilimahewa walikusanya shilingi milioni 2.
Pia
aliongeza kuwa askari polisi wakiongozwa na mkuu wa kituo cha polisi
Mirerani ASP Ally Mkalipa,walitoa sh310,000 Diwani wa kata ya Endiamtu,Lucas
Zacharia alijitolea sh3 milioni na wamiliki wa magari ya DCM walijitolea
sh360,000.
Alisema kuwa wengine waliowachangia ni marafiki
wa Diwani wao Lucas waliojitolea shilingi milioni 2 ,wafanyabiashara wa maduka
shilingi 830,000 pamoja na vifaa vilivyobambuliwa vina thamani ya
shilingi 375,000.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia,amewataka wazazi
pamoja na walezi wa kata hiyo kutoa kipaumbele pamoja na
kuzingatia kwa kuwapatia watoto wao elimu kwani kwa dunia ya sasa bila
kuwa na elimu Taifa litakuwa gizani.
“Jamani Elimu iwe ndiyo ajenda yetu ya kwanza
kwa sisi kata ya Endiamtu hivyo tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu katika
kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu bora na iliyo katika mazingira
mazuri,” alisisitiza Zacharia.
Aliendelea
kusema kuwa hivi sasa wanatakiwa kuweka nguvu moja kwenye ujenzi wa madarasa
ya shule mpya ya msingi Zaire na Endiamtu,kwani shule za msingi Mirerani na
Jitegemee hazina maeneo ya kujengewa madarasa mapya.
Amewaasa
wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo (WDC) wajitolee kwa moyo
mmoja,katika kuhakikisha kuwa wanawatumikia ipasavyo wananchi waliowachagua
kwani huu siyo wakati wa kufanya siasa.
