Na Ibrahim Yassin,Rungwe
MKUU wa wilaya Rungwe mkoani Mbeya Chrispini Meela
amefanikiwa kuumaliza mgogoro wa maji uliodumu kwa muda wa mwaka mmoja sasa
kati ya Wanananchi na mamlaka yamaji safi na taka mjini Tukuyu (TUWSA)
Mgogoro huo ulianza Agosti 8 mwaka wa 2011 ambapo mamlaka ya
maji mjini Tukuyu ilipowatangazia wateja kupanda kwa gharama za maji kutoka
sh,2000 hadi 4500 na watumiaji kufungiwa nira ambapo watumiaji hao wa maji
hawakuridhia hari hiyo na kupeleka malalamiko yao kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya
hiyo kipindi hicho Bw,Jacson Msome
Licha ya malalamiko yao kupelekwa kwa mkuu wa wilaya
hawakuweza kufikia ufumbuzi wa tatizo hilo ambapo watumiaji hoja yao kubwa
ilikuwa kwamba hawaoni sababu za kupanda bei za maji wakati miundo mbinu ya
maji ni ileile ya zamani na michakavu hakuna kilichoongezeka hivyo hawaoni
sababu ya msingi ya ongezeko hilo na kuamua kuunda umoja wa watumiaji maji wa
kata saba(MBIKI) chini ya mwenyekiti wake Watson Mwakanyamale
Mvutano huo ulikuja kuwa mkubwa na kuamua kumshirikisha mbunge
wa jimbo hilo Prof,David Mwakyusa ambapo naye aliungana na mamlaka ya maji ya
mjini Tukuyu juu upandaji wa bei na ufungaji nira ambapo watumiaji maji hao wa
maji waliamua kupeleka malalamiko yao mahakamani ambako kesi iliendelea hadi jana serikali ya
wilaya ilipoamua kuwekeana saini mbele ya Wakili Mkumbe kuwa kesi iliyopo
mahakamani ifutwe na waendelee kulipia maji
kwa bei y ash,2000 wote wenye nira na wasio na nira
Akitia saini ya makubaliano hayo mkuu huyo wa wilaya mbele
ya umati mkubwa wa Wananchi ambao ndiyo watumiaji wa maji alisema kuwa haoni
sababu za kuendelea na malumbano bali kesi iliyopo mahakamani ifutwe na
wananchi waendelee kuchangia kiasi hicho cha fedha ili mamlaka hiyo iendelee
kufanya kazi kuliko hari ilivyo hivi sasa ambapo mamlaka hiyo haikusanyi
chochote kutoka kwa watumiaji maji hasa baada ya kesi hiyo kwenda mahakamani
Alisema kwa hari hiyo sasa watumiaji wa maji sasa wamefutiwa
madeni yao yote waliyokuwa wakidaiwa wakati wa mgogoro huo wote na kuwa hata
hiyo bili ya maji y ash,2000 itaanzwa kutozwa mwezi machi mwaka huu na kuwa mkataba huo utakuwa ndani ya matazamio
kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mwezi ujao
Ukumbi wa hospitali ya wilaya Rungwe jana ulizizima kwa
furaha baada ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kuonyesha furaha kubwa huku
wakimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa
kuweza kuumaliza mgogoro huo vizuri kabisa wakati viongozi waliomtangulia
walishindwa kuutafutia ufumbuzi na kumuona kama mfalme
