Mkuu wa wilaya ya Babati Khalid Mandia amewataka
wafugaji kutokupeleka mifugo yao katika maeneo yaliyotengwa kwaajili ya ufugaji
wa nyuki.
Rai hiyo
ameitoa siku ya ugawaji wa mizinga mradi pacha wa ufugaji nyuki Mwikantsi kata
ya Mamire wilayani Babati mkoani Manyara.
Alisema kuwa maeneo hayo yaepukwe kukata miti
ovyo pamoja na kuendesha shughuli za kilimo pamoja na kuchoma ili ufugaji wa nyuki
uweze kuwa wa tija.
Aliongeza
kuwa katika ufugaji wa kisasa mizinga inapaswa itengenezewe vichanja vya urefu
wa kufika kiunoni kutoka usawa wa ardhi kufanya shughuli za ukaguzi
uvunaji wa asali na mengineyo kuwa rahisi na usihitaji watu wengi kufanya.
Aidha
aliendelea kusema kuwa serikali ya kijiji kwa kushirikiana na wanakijiji waweke
utaratibu madhubuti wa kulinda mazingira kwa faida yao pamoja na watoto wao.
Mkuu wa
wilaya huyo Khalid amesikitishwa sana na taarifa wanazozipata kutoka
TANAPA Tarangire na ofisi ya mtendaji wa kijiji kumekuwa na wimbi kubwa
la wananchi wanaovamia eneo la hifadhi kwa kuchungia mifugo na kukata miti
hovyo.
Alisema kuwa
maeneo ya hifadhi ni marufuku kufanya shughuli yeyote wakiendelea kufanya hivyo
kizazi kijacho kitabaki kuona mashamba na mifugo badala ya wanyama pori kwani
wanyama wanaposumbuliwa wanakimbilia hifadhi jirani na hatimaye wanatokomea
nchi jirani.
‘’Hifadhi
hii inafaida nyingi kwetu ikiwa ni pamoja na huduma tunazopata moja kwa moja
hapa kijijini kama shule na kuchangia pato la Taifa ,serikali ya kijiji pamoja
na wananchi tuwe mstari wa mbele katika kulinda na kutunza rasilimali
zetu.Alisema Mkuu wa wilaya Khalid.
