Inasemekana kuwa
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Shambarai Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara wametishia kuhama chama hicho kutokana na baadhi
ya viongozi wa kijiji hicho kudaiwa kuuza maeneo ya wazi bila utaratibu.
Taarifa hiyo
imetolewa na na baadhi ya wanachama hao ambao hawakutaka kutaja majina
yao kutaja majina yaowakati wakiongea na waandishi wa habari ambapo
alibainisha kuwa wamefikisha kilio chao kwa uongozi wa CCM wa kata hiyo kwa
kuwa wametokana na chama hicho lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Aidha alisema
kuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji
wa kijiji hicho,Mosses Peter wamewauzia mashamba
matajiri kutoka Arusha bila kufuata utaratibu wa kuidhinishwa na mkutano wa
kijiji.
Waliendelea
kusema kuwa viongozi hao wamefunga maeneo ya kijiji chao ikiwemo mapalio
ya kupitishia mifugo na wakihoji kwa viongozi hao kwa nini wameuza maeneo yao
wanatishiwa kwa maneno hivyo wanashindwa mahali pakwenda.
Walisema kuwa wamefikisha suala hilo hadi kwenye ofisi ya CCM ya
kata kwani viongozi hawa wametokana na CCM lakini hakuna hatua zozote
zilizochukuliwa dhidi yao.
Pia alieleza
kuwa mashamba hayo yaliyouzwa yaliachwa tangu mwaka 1975 kwa ajili ya
maeneo ya kulishia mifugo lakini wameshangazwa na viongozi hao kuamua kuyauza
kwa wafanyabiashara hao kutoka mkoani Arusha.
Kwa upande
wao mwenyekiti wa kijiji cha Shambarai Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji
hicho,Mosses Peter wamekanusha vikali kuuza maeneo hayo ila walidai kuwa
yameuzwa na wamiliki husika wa maeneo hayo.
Walisema
kuwa maeneo hayo siyo ya Serikali ila wamiliki wenyewe wameyauza mashamba
hayo ambayo ni mali yao na wao hawana mamlaka ya kuingilia au kutoa uamuzi juu
ya mashamba hayo.
Walisisitiza
kuwa wamiliki hao wameyauza kihalali mashamba hayo baada ya kupata shida
kwani kimfaacho mtu ni chake hivyo hawana uamuzi wa kumzuia kuuza kwani wenyewe
hawamiliki chochote na wala hawahusiki na mashamba hayo.
