Imebainishwa
kuwa makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013- 2014 Halmashauri ya
wilaya ya Babati mkoani Manyara inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni
33,323,868,975.00 kwamwaka wa fedha kwaajili ya kulipa mishahara ya
watumishi,matumizi mengineo na kugharimia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa
na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Dominic Kweka wakati
akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka 2013-2014 kwenye kikao cha
baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya babati kilichofanyika
Halmashaurini hapo mkoani Manyara.
Alibainisha
kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni
21,333,087,772,00 ni mapato ya vyanzo vya ndani,ruzuku ya matumizi
mengineo(oc),mishahara ya watumishi na kiasi cha shilingi bilioni
11,990,781,185.00 ni fedha za miradi ya maendeleo mbalimbali.
Pia
alitaja aina ya miradi hiyo kuwa ni mradi wa kilimo,mradi wa ukimwi,mradi wa
barabara,mfuko wa kujenga uwezo(cbg),miradi ya maendeleo(cdg),mpango wa
maendeleo ya afya ya msingi,mfuko wa afya,mpango wa maendeleo ya elimu ya
msingi na sekondari,mradi wa maji vijijini,miradi ya jamii,wadau wa maendeleo world
vision/wahisani wengine pamoja na michango ya wananchi.
Alisema
kuwa kwa upande wa matumizi Halmashauri hiyo inatarajia kutumia kiasi cha
shilingi bilioni 33,190,838,510.00 kwa mwaka wa fedha 2013-2014 kwaajili
ya kulipa mishahara ya watumishi,matumizi mengineo na kugharimu miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Aliendelea
kusema kuwa hadi mwezi disemba 2012 matumizi yote ni kiasi cha shilingi
10,195,790,0112.20 kati ya fedha hizi ni shilingi bilioni 1,214,250,276
ni matumizi ya bakaa ya mwaka 2011-2012 na shilingi bilioni 8,981,539,735.00 ni
matumizi ya bajeti ya mwaka 2011-2013 ambayo ni sawa na asilimia 39% ya lengo
ambapo katika maeneo ya matumizi kuwa ni vyanzo vya ndani vya
Halamashauri,matumizi mengineo,mishahara,mfuko wa barabara,ukarabati wa kituo
cha wazee Sarame pamoja na mfuko wa jimbo
Mkurugenzi
Kweka alitaja changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka
2012- 2013 kutokuwepo kwa mvua za kutosha kulisababisha mavuno ya mazao ya
kilimo kupungua na hivyo kuathiri ukusanyaji wa ushuru wa mazao,baadhi ya
vijiji kutokuwepo na watendaji hivyo usimamizi na utekelezaji wa shughuli za
maendeleo kukwama.
Vile vile
aliendelea kutaja changamoto zingine kuwa ni ruzuku kutoka serikali kuu
kutokufika kwa wakati au hata kutokuletwa kabisa hivyo kukwamisha utekelezaji
wa miradi iliyokusudiwa,mfumuko mkubwa wa bei ambao umesababisha gharama
huduma na bidhaa mbalimbali kupanda maradufu kama mafuta,umeme,maji,vipuri n.k.
Alisema
kuwa mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika
utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2012-2013 ni kujaza nafasi wazi za
watendaji wa vijiji,kuboresha idara ya fedha kwa kuomba ongezeko la wahasibu
pamoja na maafisa biashara pia kuongeza jhudi katika ukusanyaji wa mapato hasa
katika eneo la viwanda na kambi za kitalii na kuendelea kufuatilia na
kuikumbusha serikali umuhimu wa kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa
wakati.
