Wakati
Kenya inazihesabu siku kadhaa kufikia siku ya uchaguzi mkuu wa nchi
hiyo, serikali ya Kenya inajaribu kwa njia zote kuziba mianya yote
inayoweza kuzua hali ya machafuko kama yale yaliyotokea baada ya
uchaguzi mwaka 2007, na sasa wameangazia facebook na blogs
zinazohatarisha hali ya usalama.
Masaa
machache baada ya serikali ya Kenya kutoa onyo kwa watumiaji na
waendeshaji wa facebook pages na blogs kwa kuandika speeh ama status za
uchochezi, mapema jana wamemkamata administrator wa moja kati ya
facebook pages tano ambazo zilitajwa katika list ya kupewa onyo na
serikali hiyo.
Admin
huyo wa fan page maarufu ya "Gor Mahia is Not a Club, Its a Lifestyle.
But do we say", Collins Okello a.k.a Dr. Jarunda Jaluth Mambodiad
alikamatwa na kupelekwa katika makao makuu ya polisi kitengo cha
upelelezi (CID) kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusu status za
uchochezi kwenye page yake.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa chanzo kimoja cha kuaminika, Collins aliachiwa
baada ya mahojiano hayo. Lakini baada ya kufungwa kwa fan page hiyo,
imeanzishwa upya fan page nyingine yenye jina hilohilo "Gor Mahia is Not
a Club, Its a Lifestyle. But do we say," na hadi sasa ina LIKE zaidi ya
4, 340, ikiwa ni masaa 20 hivi baada ya kufunguliwa huku ikidrop status
inayozungumzia kufungwa kwa original fan page yao...
hii ni moja kati ya status hizo katika page hiyo..
"Jarunda was forcefully compelled to delete the original page".
Kwani ukiwa CORDed ni hate speech.Mbona page ya Stop Raila, RIP Sk Macharia etc hazijafungwa.
We
are condeming this intrusive movement of the govt, oppressing the weak n
poor, inflicting fear in them intentionally to deprive them their
constitutional rights...anyone is free to talk sense..."
Hii imekaaje kwa facebook users, ni sahihi? Toa maoni yako hapo chini
